Makini Eid Festival 2027

Siku Mbili za Faraja, Imani na Jamii

11 – 12 Machi 2027 | Siku ya Kwanza na ya Pili ya Eid

Temeke, Dar es Salaam

--Siku
--Saa
--Dakika
--Sekunde
Jiandikishe Sasa Kuwa Mdhamini

Kuhusu Tamasha

Makini Eid Festival 2027 ni tamasha kubwa la siku mbili linalolenga kujumuisha familia, vijana na wafanyabiashara. Linatarajiwa kukusanya zaidi ya watu 1,000 kutoka mkoa wa Dar es Salaam na maeneo jirani.

Tamasha hili linalenga kutoa burudani kutoka kwa waimbaji Qaswida kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar, pamoja na michezo mbalimbali ya watoto.

Dhumuni la tamasha ni kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitr 2027. Hili ni jukwaa la kijamii linalowaleta pamoja wanajamii wa rika zote ili kufurahia Eid kwa njia ya amani, upendo na maadili mema.

Tarehe

11 – 12 Machi 2027 (Siku ya Kwanza na ya Pili ya Eid)

Muda

Saa 8:00 Mchana – Saa 12:00 Jioni (Watoto)
Saa 12:00 Jioni – Saa 3:00 Usiku (Watu Wazima)

Mahali

Temeke, Dar es Salaam.

Shughuli Zilizopangwa

Qaswida Live

Jukwaa kubwa litakalowaleta pamoja waimbaji wa Qaswida kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Michezo ya Watoto

Eneo maalum la michezo kwa watoto ili kuwapa nafasi ya kufurahi katika mazingira salama na ya kimaadili.

Nasaha za Viongozi

Mafundisho kwa jamii, pamoja na hotuba kutoka kwa masheikhe na viongozi mbalimbali.

Shughuli za Hisani

Zawadi kwa yatima na matembezi ya hisani kwa wagonjwa hospitalini wakati wa Ramadhani.

Vifurushi vya Udhamini

Chagua kifurushi kinachokufaa ili bidhaa na huduma zako zifikie maelfu ya wateja. (Nafasi ni chache, zinajazwa kwa mfuatano wa kuthibitisha)

PLATINUM

TZS 10,000,000/=
Nafasi 1 Pekee
  • Nembo kubwa zaidi kwenye jukwaa kuu
  • Banda kubwa la maonesho
  • Mwakilishi kuzungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari
  • Hotuba dakika 20 siku zote mbili
  • Mdhamini Mkuu wa tamasha (Atatajwa kwenye matangazo yote)
  • Mahojiano maalum manne kwenye vyombo vya habari
  • Cheti cha kutambuliwa na cheti cha shukrani
  • Nembo kwenye T-shirts za kamati
  • Roll-up banner 6 + Vipeperushi
  • Mwakilishi atakuwepo sehemu ya VIP

GOLD

TZS 6,000,000/=
Nafasi 2 Pekee
  • Nembo ya saizi ya kati kwenye jukwaa
  • Kuonekana katika mabango ya mahojiano
  • Kutajwa na MC
  • Mdhamini atatajwa kwenye tangazo la tamasha
  • Banda la maonesho
  • Dakika 10 za salamu rasmi
  • Mahojiano mawili na vyombo vya habari
  • Nembo kuonekana katika mabango ya tamasha
  • Cheti cha shukrani na cheti cha Mdhamini
  • Roll-up banner 4
  • Mwakilishi atakuwepo sehemu ya VIP

SILVER

TZS 3,000,000/=
Nafasi 3 Pekee
  • Kutajwa kama sehemu ya wadhamini
  • Kutajwa katika matangazo ya radio na mitandao
  • Banda la maonesho
  • Nembo katika mabango ya washirika
  • Mahojiano mawili katika vyombo vya habari
  • Dakika 5 za salamu rasmi
  • Cheti cha shukrani na cheti cha Mdhamini
  • Roll-up banner 2
  • Mwakilishi atakuwepo sehemu ya VIP

BRONZE

TZS 1,000,000/=
Nafasi Nyingi
  • Nembo kuwekwa kwenye bango la washirika
  • Utangazaji kwenye kurasa za kidijitali
  • Post katika mitandao ya kijamii
  • Kutajwa na MC katika tamasha
  • Mahojiano moja na vyombo vya habari
  • Dakika 3 za salamu rasmi
  • Cheti cha Mdhamini
  • Mwakilishi atakuwepo sehemu ya VIP

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je, kuna kuingia bure?

Maelezo kuhusu kiingilio yatatangazwa hivi karibuni. Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa zaidi.

Je, kuna maegesho?

Maelezo ya maegesho yatatangazwa hivi karibuni. Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii.

Je, naweza kushiriki kama mdhamini?

Ndiyo! Tazama sehemu ya "Vifurushi vya Udhamini" hapo juu au wasiliana nasi kupitia WhatsApp kwa maelezo zaidi.

Je, ninawezaje kuwa mfanyabiashara kwenye tamasha?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp au barua pepe ili tupange nafasi ya banda la maonesho.

Je, kuna shughuli za hisani?

Ndiyo — tunapanga zawadi kwa yatima na matembezi ya hisani kwa wagonjwa hospitalini wakati wa Ramadhani. Wasiliana nasi kama unataka kushiriki.

Jiandikishe / Omba Udhamini

Jaza fomu hii ili tukuwasiliane. Usajili ni bure.

Bofya kitufe hapa chini kufungua fomu yetu. Itakuchukua sekunde chache kujaza.
📝 Jaza Fomu Sasa

Itafunguka kwenye ukurasa mpya

Mawasiliano

Tuko tayari kufanya kikao nasi ana kwa ana au mtandaoni ili kueleza mchanganuo huu kwa kina na kurekebisha kifurushi kulingana na mahitaji yako.


Barua Pepe: masoko@makiniforums.co.tz

Simu: 0733 354 060

Anuani: S.L.P. 5265, Dar es Salaam

Waandaaji: Makini Forums

Malipo

Malipo yote ya udhamini na ihsani yanaweza kufanyika kupitia akaunti rasmi ya Makini Forums:

CRDB Bank

Jina la Akaunti: Makini Forums

Namba ya Akaunti: 10554325144

Tawi: Uhuru Branch, Dar es Salaam

Baada ya malipo, wasiliana nasi kupitia WhatsApp au Barua Pepe kwa uthibitisho na risiti.

💬 ↑